+255 (0) 759 156 716 saintgabriel2017@gmail.com

St. Gabriel Technical Secondary School

"Solution for Technical challenges"

Logo
St. Gabriel Technical Secondary School

Overview

ST. GABRIEL TECHNICAL SECONDARY SCHOOL

Elimu Bora • Ufundi Stadi • Malezi Bora • Maandalizi ya Maisha

St. Gabriel Technical Secondary School ni shule ya sekondari ya ufundi inayomilikiwa na Mapadri wa Passionist, yenye dhamira ya kutoa elimu bora ya kitaaluma, ufundi na malezi kwa vijana ili kuwaandaa kwa maisha, ajira na kujiajiri.

Shule inatangaza nafasi za masomo kwa Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2027, na inawakaribisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika mazingira bora ya kujifunzia na kujenga vipaji.

  • Shule ya Kutwa na Bweni

St. Gabriel inapokea wanafunzi wa jinsia zote — wavulana na wasichana — kutoka dini zote, hivyo kutoa fursa sawa ya elimu kwa vijana kutoka familia na imani mbalimbali.

  • Elimu ya Ufundi kwa Vitendo

Moja ya sifa kuu za St. Gabriel ni msisitizo katika elimu ya ufundi na ujuzi wa vitendo. Shule ina mazingira na maabara/workshops zinazowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kukuza vipaji vyao katika maeneo mbalimbali ya ufundi.

Wanafunzi wanapata fursa ya kutumia maabara na karakana bora za ufundi, pamoja na kujifunza stadi zinazoweza kuwasaidia katika kuendelea na elimu ya juu, kupata ajira au kujiajiri.

  • Maabara Bora za Sayansi

Shule inaweka mkazo pia katika masomo ya sayansi kupitia maabara nzuri na mazingira yanayomuwezesha mwanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo. Hii huwasaidia wanafunzi kuelewa dhana za kisayansi kwa ufanisi zaidi na kujiandaa kwa masomo ya juu.

  • Mazingira Mazuri ya Kujifunzia

St. Gabriel imejengwa katika mazingira mazuri, salama na yenye mandhari ya kuvutia, yanayomuwezesha mwanafunzi kusoma, kuishi na kukuza vipaji vyake katika mazingira yenye utulivu.